Eid Mubarak!
Tanzania Investment Centre
Investment Management
First Point of Call for investors in Tanzania. Promotes, facilitates and coordinate investment activities in the country
About us
TIC is the First point of call for all investors interested to invest in the country. The Government of Tanzania established Tanzania Investment Centre (TIC) through an Investment Act with the core function of coordinating, encouraging, promoting and facilitating investment in Tanzania, and has the role to advise the Government on investment policy and related matters. Investors are facilitated to access investment approvals, necessary permits, registration and licenses under One Stop Facilitation Centre.
- Website
-
http://www.tic.go.tz
External link for Tanzania Investment Centre
- Industry
- Investment Management
- Company size
- 51-200 employees
- Headquarters
- Dar-es-salaam
- Type
- Government Agency
- Founded
- 1997
Locations
-
Primary
Dar-es-salaam, TZ
Employees at Tanzania Investment Centre
-
Peter Chisawillo
-
Anna Lyimo-Kessy
Research and Planning Manager - Tanzania Investment Centre
-
RAHABU SAKILALI
ICT Policy Developer | Advisor in Digital Transformation and Cybersecurity Solutions
-
Amne Suedi
Africa's Pickiest Investment Adviser - Unlocking Investment Opportunities Across Switzerland, Africa and the World. Facilitating Partnerships…
Updates
-
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Mipango na Uwekezaji, Mhe. Prof. Kitila Mkumbo (Mb), ameshiriki katika hafla maalum ya Iftar pamoja na wawekezaji mbalimbali nchini. Hafla hiyo imefanyika leo Machi 27, 2025, katika ukumbi wa Ubungo Plaza, jijini Dar Es Salaam, iliyoandaljwa kwa ushirikiano kati ya Kituo cha Uwekezaji Nchini (TIC) na Taasisi ya Sekta Binafsi Nchini (TPSF). Prof. Kitila amewapongeza wawekezaji kwa juhudi kubwa wanazoendelea kuzifanya katika kuimarisha uchumi wa nchi. Amehaidi kuwa serikali itaendelea kushirikiana nao kutatua changamoto wanazokumbana nazo katika shughuli zao za uwekezaji. Hafla hiyo pia ilihudhuriwa na Mhe. Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Lazaro Twange, Mtendaji Mkuu wa TIC, Gilead Teri, na Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF, Raphael Maganga pamoja na wawekezaji na wafanyabiashara kutoka sekta mbalimbali pamoja na viongozi wa dini na wa kisiasa kutoka Wilaya ya Ubungo.
-
-
-
-
-
+1
-
-
Leo Machi, 26 , 2025, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Mipango na Uwekezaji, Mhe. Prof. Kitila Mkumbo, amesisitiza dhamira ya serikali ya kuhakikisha kuwa uwezeshaji wa wawekezaji nchini unafanyika kwa ufanisi kupitia Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC). Aidha, ameeleza umuhimu wa kuboresha miundombinu ili kuhakikisha kuwa shughuli za kiuchumi zinaendelea bila vikwazo vyovyote. Waziri Prof. Mkumbo alitoa kauli hiyo wakati alipokuwa kwenye ziara ya kutembelea miradi mbalimbali katika mkoa wa Pwani. Akizungumza na waandishi wa habari akiwa katika mradi wa Kinglion, alisisitiza kwamba serikali inafanya kazi kwa bidii kuondoa vikwazo vya uwekezaji.
-
NJOMBE📍 Akiwa katika ufunguzi wa Ofisi ya TIC Kanda ya Nyasa, Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe. Anthony Mtaka alieleza dhamira ya kushirikiana na Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kuhakikisha kwamba Watanzania wanaowekeza katika mkoa huo wanapata huduma bora na sahihi. Mhe. Mtaka alisisitiza kwamba kati ya fursa zilizopo mkoani Njombe ni pamoja na kuongeza thamani mazao ya parachichi, misitu na mahindi ili kuongeza ajira kwa vijana wanaohitimu katika shule na vyuo mbalimbali nchini. Katika hotuba yake, Mhe. Mtaka alieleza kwamba mkoa wa Njombe umetekeleza kwa vitendo maono ya Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jumhuri ya Tanzania kwa kuhakikisha Watanzania wanashiriki kikamilifu katika uchumi wa nchi yao kwa kuwekeza katika sekta mbalimbali kupitia fursa zilizopo katika mkoa wa Njombe. Aliongeza kuwa, kusogeza huduma za uwekezaji katika mikoa hiyo kunalenga kuwawezesha wawekezaji wa ndani kupata huduma bora zaidi, kuwatatulia changamoto zao kwa haraka na kuwawezesha katika uwekezaji wao. Sambamba na uzinduzi wa ofisi hiyo, Mhe. Mtaka aliandaa ziara kwa ajili ya Mhe. Prof. Kitila Mkumbo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Mipango na Uwekezaji ambaye alikuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa ofisi hiyo ya TIC , Prof. Kitila ajionee miradi inayomilikiwa na Watanzania katika mkoa wa Njombe ili kuona jinsi gani serikali inaweza kusaidia katika kufanikisha miradi hiyo.
-
-
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo, ametoa wito kwa taasisi za serikali kuweka vipaumbele katika kuboresha miundombinu, hasa katika maeneo yenye vyanzo vya kiuchumi kama vile maeneo ya uwekezaji. Aliyasema haya mapema jana baada ya ufunguzi wa ofisi ya Kanda ya Nyasa ya Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) iliyoko Njombe. Prof. Mkumbo alizungumza akiwa katika kiwanda cha Murikado Food Supply Co. Ltd, kilichopo Makambako ambacho kinamilikiwa na Mtanzania aliyewekeza kiasi cha shilingi bilioni 5 za kitanzania kinachochakara mafuta ya parachichi mkoani humo. Alisisitiza kuwa huduma za msingi kama maji, barabara, na umeme ni muhimu mno kwa mwekezaji, ambaye hapaswi kuhangaika kuhusu huduma hizi, kwani anakuja kuzalisha ajira na kuchangia katika ukuaji wa uchumi wa eneo husika. Aliendelea kwa kumpongeza mwekezaji huyu, ambaye ni Mtanzania aliyewekeza na kuona fursa katika sekta ya kilimo hadi uchakataji wa mafuta. Pia alibainisha kuwa Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anafurahishwa kuona Watanzania wajasiri kama hawa wanaothubutu na kuchangia katika ukuaji wa uchumi wa nchi.
-
-
Katika juhudi za kuboresha mazingira ya uwekezaji nchini, serikali imejizatiti kuhakikisha inatoa huduma bora kwa wawekezaji wote. Haya yamesemwa na Mhe. Prof. Kitila Mkumbo alipokuwa akizungumza na wawekezaji katika hafla ya ufunguzi wa ofisi mpya ya Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Kanda ya Nyasa, mkoani Njombe. Prof. Kitila amesisitiza umuhimu wa TIC kutoa huduma bora na za kina kwa wawekezaji katika kanda hii. Alitoa agizo kwa TIC kuhakikisha kuwa wawekezaji hawakumbani na changamoto zisizo za lazima katika shughuli zao za uwekezaji. Amewataka washirikiane na ofisi za halmashauri ili waweze kuwasaidia wawekezaji kwa ufanisi zaidi. Ufunguzi huu ni sehemu ya juhudi za serikali kuboresha mazingira ya uwekezaji nchini na kuhakikisha kuwa maono ya Mhe. Rais ya kusogeza huduma karibu zaidi na Watanzania ambao wamewekeza au wana nia ya kuwekeza yanatimia. Hafla hii muhimu ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa mkoa wakiongozwa na Mhe. Anthony Mataka, Mkuu wa Mkoa wa Njombe. Pia walikuwepo Mwenyekiti wa Bodi ya TIC, Mkurugenzi Mtendaji wa TIC Gilead Teri, pamoja na wakuu wa wilaya za mikoa husika, wawekezaji, na wafanyabiashara wa mkoa wa Njombe.
-
-
-
-
-
+1
-
-
Enhancing the investment landscape for Tanzanians, the government under the leadership of President Dr. Samia Suluhu Hassan is strengthening opportunities for local investors by providing excellent services and ensuring an optimal investment environment. Today, March 24, 2025, the Tanzania Investment Centre (TIC) proudly announces the official opening of the new Nyasa Zone office in the Njombe region. This office will cater to the regions of Njombe, Ruvuma, Iringa, and Mtwara, focusing on delivering exceptional services to local investors and facilitating closer access to opportunities. Hon. Prof. Kitila Mkumbo, the Minister of State, President's Office - Planning and Investment, will grace the opening ceremony as the guest of honor. During his visit, he will also tour various investment projects and engage with investors, aiming to further enhance the investment climate in the region. We are confident that this new office will greatly enhance local investment and drive economic growth both within the region and across the nation.
-