𝐔𝐬𝐢𝐦𝐚𝐦𝐢𝐳𝐢 𝐰𝐚 𝐌𝐢𝐫𝐚𝐭𝐡𝐢 𝐓𝐚𝐧𝐳𝐚𝐧𝐢𝐚 Kutokuwa na ulewa wa taratibu za kusimamia na kugawa mali za marehemu kwa warithi wake katika jamii ndio chanzo cha matatizo makubwa ambayo hujitokeza katika familia/ukoo pale mtu anapofariki. Mgawanyo wa mirathi hutegemea mwenendo wa maisha ya marehemu kabla ya kifo. Ili kuweza kutambua ni sheria gani itumike katika utaratibu wa urithi na mirathi sheria zifuatazo huzingatiwa: 1. Sheria za kiserikali 2. Sheria za kiislamu 3. Sheria za kimila Ili kulinda na kutunza mali za marehemu ni lazima shauri la mirathi lifunguliwe kulingana na sheria itakayosimamia mirathi husika pamoja na kuambatanisha nyaraka zote muhimu ikiwa ni pamoja na cheti cha kifo cha marehemu: 1. Shauri la mirathi linalohusu sheria za kimila au sheria za kiislam litafunguliwa katika mahakama ya Mwanzo. 2. Shauri la mirathi linalohusu sheria za kiserikali linashughulikiwa au kufunguliwa katika mahakama ya wilaya au hakimu mkazi ama mahakama kuu. Ili msimamizi wa mirathi aweze kupata barua ya usimamizi wa mirathi kutoka mahakamani ni lazima awe ameteuliwa na wosia ama katika kikao cha familia/ukoo. Msimamizi wa Mirathi atatakiwa kukusanya mali zote za marehemu ikiwa ni pamoja na fedha, mali isiyohamishika na zinazohamishika na mali nyingenezo za marehemu. Pia msimamiz wa mirathi atatakiwa kuhahikisha analipa madeni yote ya marehemu kabla ya kugawa mali kwa warithi. Mwisho msimamizi wa mirathi anapaswa kuwasilisha ripoti ya mgawanyo wa mali kwa mahakama ndani ya muda alipewa katika barua ya usimamizi wa mirathi na kufunga shauri hilo la mirathi kwa wakati. #Mirathi #Sheria #LawficAttorneys #DarEsSalaam #Tanzania