Women And Youth Movement (woyomo)’s Post

Mambo vipi rafiki! Tuna habari njema kwaajili yako kijana, leo tunazindua rasmi mradi wetu wa Health Spark wenye lengo la kutoa elimu ya afya ya uzazi na ujinsia kwa vijana wa kitanzania. Awamu hii tutaanza na vijana wa Dar es Salaam, na mradi huu utahusisha vijana katika utekelezaji wake ikiwemo kwenye kuamua maeneo ya Dar es Salaam yakuanza nayo, lakini pia Tutawapa vijana nafasi ya kuwa walimu wa taarifa sahihi za afya ya uzazi kwa vijana wenzao. Tukiamini katika nguvu ya vijana katika kuleta mabadiliko ya vijana wenzao, hivyo tutatoa nafasi ya vijana waliotayari kujitolea kuwa Peer Educators chini ya mradi huu. Kaa tayari kwa taarifa zaidi, na kama wewe ni mdau wa mabadiliko ya vijana wenzako hii ni kwaajili yako. Sisi tunasema “Hakuna kitu cha vijana, Pasipo Vijana”. #Afyayauzazinihaki

  • No alternative text description for this image

To view or add a comment, sign in

Explore topics