Kupitia Makubaliano ya Kibiashara kati yetu na Puma, hivi karibuni tumeshiriki katika Mkutano wa wasambazaji wa mafuta wa Puma na kuwakilishwa na Bi. Jacqueline Michael, Meneja wa Mapendekezo ya Wateja. Pamoja na wafanyakazi wetu wengine, tuliweza kuelezea mpango wetu wa kendelea kuwahudumia na kutatua changamoto zao mbalimbali katika mnyororo wa thamani wa sekta hii ya mafuta. Kama benki inayolenga kutoa suluhisho kwa wasambazaji, tumejizatiti kukidhi mahitaji ya wateja wetu kwa kutoa huduma maalum kwa ajili ya kusaidia ukuaji wa biashara zao.
-
+1