Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya PURA Bw. Halfani Halfani ameipongeza Mamlaka kwa kuratibu uandaliwaji wa miongozo ya Uwajibikaji wa Kampuni kwa Jamii (CSR) katika mamlaka za serikali za mitaa kwa maeneo inapotekelezwa miradi ya utafutaji, uendelezaji na uzalishaji wa mafuta na gesi asilia Pamoja na Yale yaliyopitiwa na mondo mbinu ya gesi asilia. Aidha ametoa rai kwa PURA kushirikiana na Mamlaka ya Huduma za Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA) katika kuhakikisha miradi ya CSR inanufaisha wazawa katika miradi ya sekta ndogo ya mafuta na gesi asilia kwa ngazi za mkondo wa juu, wa kati na wa chini Bw. Halfani ameyasema hayo leo Julai 11, 2024 alipotembelea banda la PURA katika Maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba) yanayoendelea kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere jijiji Dar es Salaam. Mbali na banda la PURA Bw. Halfani ametembelea mabanda mengine ya taasisi zilizo chini ya Wizara ya Nishati ikiwemo Mamlaka ya Huduma za Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA), Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC) na Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) pamoja na Mamlaka ya Udhibiti wa Utafutaji na Uchimbaji wa Mafuta na Gesi Asilia Zanzibar (ZPRA) ili kupata uelewa zaidi wa shughuli zake na miradi wanayoitekeleza.
-
-
-
-
-
+1